Tunu Pinda Youth Foundation Yatembelea Shule ya Majimoto Maalum Msingi na Kufanya Tendo la Hisani (Charity)

0 Comments

Mnamo tarehe 22 Novemba 2024. TUNU PINDA YOUTH FOUNDATION ilifanya ziara ya kutembelea Watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya msingi Maji moto Maalum. Safari hiyo iliambata na michango ya wahisani kutoka TUNU PINDA YOUTH FOUNDATION na wadau wengine ambao walipenda kuungana na Taasisi. Jumla ya kiasi kilichokusanywa ni Shilingi lakin sita na elfu saba tu (Tsh 607,000/=) ambazo zilitumika kununua baadhi ya mahitaji ya kusomea na kujifunzia kama vile madaftari, kalamu za kuandikia, Rim paper, notebook na diary kwa ajili ya walimu. Fedha nyingine zilitumika kwa ajili ya kununua viburudisho kwa ajili ya Watoto.

Ujio wa hisani hii uliambatana na Safari ya kutembelea hifadhi ya mbuga ya KATAVI iliyopo katika mkoa wa Katavi. Mbuga ya Katavi ni mbuga ya tatu kwa ukubwa katika mbuga zote Tanzania. Watoto walifurahi kuwaona Wanyama kama Tembo, Twiga, Mamba, Kiboko, Swala, Nyati na Ngiri. Baada ya kumaliza kutembelea hifadhi Wanafunzi wakiambatana na wajumbe wa TUNU PINDA YOUTH FOUNDATION Pamoja na walimu wao walirejea shuleni na kukabidhiwa mahitaji yote muhimu japo kwa uchache yaliyonunuliwa na Taasisi.

 

Mwenyekiti wa Tunu Pinda Youth Foundation kwa niaba ya Taasisi alimshukuru Mwenyeji wetu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Pinda ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mwenyekiti alimshukuru Naibu wa Waziri kwa kutukaribisha Jimboni kwake lakini pia kuturuhusu kufika katika Shule ya Msingi Majimoto Maalum kwa ajili ya kufanya tendo la huruma. Mwenyekiti aliwashukuru wanachama na wadau wote waliowezeshe kupatikana kwa michango hiyo kwa ajili ya Watoto wetu.

Mwenyekiti kwa niaba ya TPYF alitumia nafasi hiyo Kumshukuru Mkurugenzi wa Halmashaur ya Mpimbwe kwa kukubali Taasisi kutembelea shule iliyo chini ya Idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari, Kwanza kabisa kwa kutupatia kibali cha kutembelea shule hiyo na pia kuwaruhusu wanafunzi na walimu wao kuambatana na Taasisi kuelekea mbuga za Wanyama za Katavi ili kuwajenga Watoto katika hali ya udadisi kwa kuwaona Wanyama kwa uhalisia wao.