Warsha ya Siku ya Mtoto wa Kiume wa Daktari Samia

0 Comments

Tunu Pinda Youth Foundation inalenga kuongeza uelewa kwa jamii kupitia warsha za kujenga uwezo ili kuimarisha ushiriki wa vijana katika matukio ya kitaifa nchini Tanzania.

Kwa kutambua changamoto wanazokutana nazo watoto wa kiume katika familia, shuleni, na jamii kwa ujumla; taasisi iliandaa warsha ya siku moja tarehe 11 Juni 2024, iliyojulikana kama “SIKU YA MTOTO WA KIUME WA DAKTARI SAMIA.” Warsha hiyo iliwashirikisha watoto wa kiume wa darasa la nne hadi la saba kutoka shule 10 za msingi jijini Dodoma pamoja na walimu wao.

Wanachama wa taasisi waliyopata mafunzo maalumu walizungumza na watoto hao ili kutambua changamoto zao na kuwasaidia kujitambua. Aidha, kulifanyika maandamano kutoka Nyerere Square kuelekea ukumbi wa Cathedral (Roma) Dodoma, wakiwa na mabango yanayolaani ukatili dhidi ya watoto wa kiume.

Taasisi inalenga kufanya hili kuwa juhudi endelevu na kuwafikia wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu katika kipindi cha miaka mitano.